Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Alasiri ya leo Jumatano mwezi (1 Dhulhijjah 1441h) sawa na tarehe (22 Julai 2020m) umetoa maelezo kuhusu kuuwawa kwa kijana Ghazwani Baasim Sirriy, ifuatayo ni nakala ya tamko hilo:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.
Atabatu Abbasiyya imepokea kwa huzuni kubwa taarifa ya kifo cha kijana Ghazwani Baasim Sirriy kilicho tokana na utovu wa nidhamu wa baadhi ya askari wa kitengo cha nidhamu, kikosi cha mkanda wa kijani, ambacho wapo chini ya idara ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa zaidi ya miaka mitatu kinashirikiana na jeshi la wananchi, kulinda mali za umma na binafsi, ilikuja gari ghafla ikiwa na vijana watatu saa tano usiku, askari wa zamu walipo wakaribia vijana hao wakakimbia, jambo lililopelekea mmoja wa askari kuwafyatulia risasi iliyo mjeruhi mmoja wa vijana hoa na kusababisha kifo chake (Mwenyezi Mungu amrehemu).
Tunaipa pole familia ya marehem.. na tunamuomba Mwenyezi Mungu amuingize peponi na aipe subira na uvumilivu familia yake.
Tambua kuwa askari wa zamu walimpeleka hospitali kijana aliye jeruhiwa wakati huohuo, na akafariki baada ya kufikishwa hospitalini (Allah amrehemu), na wakajisalimisha kwenye vyombo vya usalama ili muuwaji aadhibiwe kwa mujibu wa sheria, tuiachie mahakama itatoa hukumu kwa kufuata sheria kutokana na ushahidi walio nao.
Ataba inasisitiza kuwa hiki ni kitendo cha mtu binafsi aliye sababisha kifo, Ataba tukufu haijatoa agizo la kufyatua risasi kwa mtu yeyote, jambo hilo linahusika na vyombo vya ulinzi na usalama pekeyake, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu alilinde taifa letu na wananchi wetu kutokana na kila baya hakika yeye ni mwingi wa kusikia na mwingi wa kujibu…
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu
1 Dhulhijjah 1441h
22 Julai 2020m.