Kamera za ulinzi zilizo fungwa kwenye eneo linalo zunguka Atabatu Abbasiyya tukufu kwa nje zina ubora na uwezo mkubwa

Maoni katika picha
Idara ya mawasiliano na teknolojia chini ya kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya imekamilisha ufungaji wa kamera za ulinzi kwenye eneo linalo zunguka haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa nje, zenye uwezo wa kuona tukio lolote la uvunjifu wa amani unao weza kutokea.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kiongozi wa idara hiyo Mhandisi Farasi Abbasi Hamza, akaongeza kuwa: “Idara yetu kupitia watumishi wake wenye ujuzi na uzowefu mkubwa katika sekta hii, inajitahidi kwenda sambamba na maendeleo ya sekta ya kamera za ulinzi, hivi karibuni tumemaliza kufunga kamera (60) za kisasa zenye ubora mkubwa, kwenye eneo linalo zunguka Atabatu Abbasiyya tukufu, katika sehemu za kuvulia viatu (Kashwaniya) na sehemu za kutunzia vitu (Amanaat) sambamba na maeneo ya funguo za masanduku ya kutunzia vitu (Amanaat) yanayo zunguka Atabatu Abbasiyya pande zote nne, kamera hizo zinaonyesha kila kitu kwenye maeneo hayo na maeneo jirani”.

Akaongeza kuwa: “Sehemu hizo wakati wa ziara zinazo hudhuruwa na mamilioni ya watu huwa na misongamano mikubwa, kamera zilizokuwepo awali zilikuwa haziwezi kuonyesha kila kitu, kutokana na umuhimu wa kuhakikisha watu wanaoingia katika maeneo hayo wanapata huduma bora, na wanatembea bila tatizo, tumefunga kamera hizi ambazo zitasaidia kumhudumia zaairu pamoja na mtumishi wa Ataba”.

Akasisitiza kuwa: “Mradi wetu haujaishia kwenye kufunga kamera za kisasa peke yake, bali kunamkakati mwingine kuhusu majengo ya chini na huduma watakazo pewa mazuwaru kwenye maeneo hayo, kamera hizo zimeunganishwa na mfumo mkuu wa ulinzi katika Atabatu Abbasiyya na kwenye vyumba vya ukaguzi, sambamba na kufunga tv (screen) katika kitengo cha utumishi kinacho simamia utowaji wa huduma kwa mazuwaru”.

Akamaliza kwa kusema: “Kazi imekamilika ndani ya muda uliopangwa na imefanywa na watumishi wa idara yetu bila kusaidiwa na watu wa nje, siku za nyuma kazi za aina hii zilikuwa zinaigharimu hela nyingi Atabatu Abbasiyya tukufu, tumefanya majaribio na yameonyesha mafanikio makubwa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: