Kikosi cha Abbasi kimesema kuwa: Mwananchi anaweza kuzika ndugu yake aliye kufa kwa Korona kwenye makaburi yao maalum

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdu-Shaábi) kimesema kuwa mwananchi anaweza kumzika ngugu yake aliyekufa kwa maradhi ya Korona kwenye makaburi yao maalum, maadam shughuli za mazishi ziwe chini yetu na baada ya kupata kibali rasmi kutoka kwenye sekta zinazo husika.

Idadi ya watu walio oshwa na kuzikwa na kikosi hicho imefika (22), wanaume (15) na wanawake (7) tangu kilipo funguliwa kituo cha kushughulikia mazishi ya watu waliokufa kwa janga la Korona.

Kwa kuwasiliana na kikosi cha uoshaji piga namba zifuatazo:

Amniyya/ 07602421477

Asiya/ 07728941666

Al-Athiir/ 07806196550

Tambua kuwa wakati wa kazi ni saa (2) jioni hadi saa (11) asubuhi.

Kumbuka kuwa kituo hiki ni kwa ajili ya watu waliokufa kwa janga la Korona, kipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimejengwa kutokana na agizo la kiongozi mkuu wa kisheria wa Ataba Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, kufuatia maombi ya wananchi, na kikosi cha Abbasi ndio kinasimamia shughuli za mazishi, kipo kwenye eneo la makaburi mapya ya Karbala katika kiwanja chenye ukubwa wa mita (3750), chumba cha kuoshea maiti kina ukubwa wa mita (120), kinasehemu mbili, ya wanaume na wanawake, chumba hicho kinavifaa vyote vinavyo hitajika katika uoshaji na upambaji wa mtu aliyekufa kwa janga la Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: