Kikosi cha Abbasi kinaendelea kutoa huduma za matibabu kwa watu walio ambukizwa virusi vya korona waliopo karantini

Maoni katika picha
Kikosi cha kujibu haraka cha madaktari katika mji wa Bashiri chini ya kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdu-Shaábi) kinaendelea kutoa huduma za matibabu kwa watu walio ambukizwa virusi vya Korona waliopo karantini siku saba mfululizo, kwa kushirikiana na kitengo cha dharura cha idara ya afya ya Karkuuk.

Utaratibu huu upo katika mkakati maalum wa kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa wa Korona kupitia wawakilishi wake waliopo kwenye mikoa tofauti hapa nchini.

Katika mji wa Waasit kunakikosi kazi cha madaktari kinacho tibu watu walio ambukizwa Korona, wameshafanya program nyingi kwenye vitongoji tofauti vya mji huo, msemaji wa kikosi ameripoti kuwa kikosikazi kinaundwa na madaktari mahiri wenye uzowefu wa kuwatibu watu waliopo karantini, na wanafanya hivyo kwa kushirikiana na kituo cha afya cha Waasit.

Akaongeza kuwa: Kikosi kinatoa matibabu na mitambo ya Oksijen kwa wagonjwa sambamba na kuchukua hatua zote za kujikinga na maambukizi kwa ajili ya usalama wao.

Kumbuka kuwa kikosi kiliunda kamati maalum ya kupambana na janga la Korona, kamati hiyo imesha fanya program nyingi, hususan katika maeneo yenye wakazi wengi ndani na nje ya mji wa Karbala, inafanya kila iwezalo katika kupambana na janga hilo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: