Idara ya uhusiano wa vyuo vikuu na shule imefanya warsha kuhusu changamoto kubwa anayopata mwanafunzi katika mtihani wa kwenye mtandao

Maoni katika picha
Idara ya uhusiano wa vyuo na shule katika Atabatu Abbasiyya Alasiri ya Ijumaa mwezi (3 Dhulhijjah 1441h) sawa na tarehe (24 Julai 2020m), imefanya warsha kwa wanafunzi wa vyuo na maahadi iliyokuwa na anuani isemayo: (usomaji kwa njia ya mtandao katika vyuo vikuu vya Iraq na changamoto kubwa anazo pata mwanafnzi kwenye mtihani anaofanya kwa njia ya mtandao) warsha hiyo imeendeshwa kwa kutumia programa ya (Moodle) na (Google Classroom).

Tumeongea na kiongozi wa harakati za vyuo kuhusu warsha hiyo, Sayyid Muntadhar Swafi amesema kuwa: “Lengo la warsha hii ni kufafanua namna ya kutumia program za mitandao katika kufanya mtihani wa mwisho wa mwaka chini ya maazimio ya wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu”.

Warsha hii ni miongoni mwa warsha nyingi zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara tajwa chini ya kitengo cha mahusiano, kutokana na mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa, inalenga kutatua changamoto kubwa ambayo wanapata wanafunzi kwenye mtihani wa mwisho, pamoja na kujibu maswali yao.

Kumbuka kuwa idara ya uhusiano wa vyuo na shule ni miongoni mwa idara zilizo chini ya kitengo kikuu cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: