Zaidi ya mazuwaru 116 eflu wamefanyiwa ziara kwa niaba ndani ya mwezi mtukufu wa Dhulqaada

Maoni katika picha
Dirisha la ziara kwa niaba katika mtandao wa kimataifa Alkafeel limefanyia ziara jumla ya watu (116,141) walio jiandikisha ndani ya mwezi wa Dhulqaada kutona nchi tofauti duniani kupitia toghuti zake za (kiarabu, kiengereza, kifarsi, kituruki, kiurdu, kifaransa, Kiswahili na kijerumani).

Kwa mujibu wa maelezo ya Ustadh Haidari Twalib Abdul-Amiir kiongozi wa idara ya teknik na mitandao ya Atabatu Abbasiyya tukufu, amesema: “Kufanya ziara kwa niaba ni miongoni mwa huduma zinazo tolewa na mtandao wa kimataifa Alkafeel, kunashuhudia kuongezeka kwa watu wanaojisajili siku baada ya siku, hususan katika mazingira ya sasa ya maambukizi ya virusi vya Korona, ambayo yamepelekea kuzuwia watu wengi kuja kufanya ziara kwenye maeneo matakatifu”.

Akabainisha kuwa: “Mwezi wa Dhulqaada umeshuhudia ziara nyingi, miongoni mwa ziara hizo ni:

  • - Ziara ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kila usiku wa Ijumaa, pamoja na ziara ya kila siku ya Abulfadhil Abbasi (a.s), zimefanywa na idara ya masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya.
  • - Ziara ya bibi Maasumah binti wa Imamu Mussa bun Jafari (a.s) katika mji wa Qum, katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, imefanywa na watu walio jitolewa mbele ya malalo yake takatifu.
  • - Ziara ya Imamu Ali bun Mussa Ridhwa (a.s) katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, imefanywa na watu waliojitolea mbele ya malalo yake takatifu.
  • - Ziara ya Imamu Muhammad Baaqir (a.s) katika kumbukumbu ya kifo chake, imefanywa na watumishi wa malalo ya maimamu wawili Jawadaini katika mji wa Kadhimiyya”.

Akaendelea kusema: “Kulikuwa na muda mrefu wa kutangaza ziara hizi, ili kutoa nafasi ya kujisajili watu wengi zaidi, asilimia kubwa ya watu walio jisajili wametoka katika nchi zifuatazo: (Iraq, Iran, Lebanon, Pakistan, Urusi, Marekani, Uingereza, India, Saudia, Swiden, Kanada, Kuwait, Malezia, Australia, Algeria, Baharain, Misri, Ujerumani, Island, Namsa, Yunani, Holandi, Tunisia, Denmak, Norwey, Qatar, Ubelgiji, Moroko, Afughanistan, Oman, Ekowad, Brazili, Ajentina, Uswisi, Naijeria, Gana, Yemen, Indonesia, Italia, Hispania, Ufaransa, Uturuki, Adharbaijan, Qabras, Finlad, China, Ealende, Honkon, Japani, Imarati, Sudani)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: