Idara ya mkoa wa Diyala inafanya msafara ya kwenda kuwasaidia wapiganaji walipo katika mkoa wa Samara na kwenye mgahawa (mudhifu) wa maimamu wawili Askariyyaini

Maoni katika picha
Idara ya mkoa wa Diyala chini ya kitengo cha ustawi wa jamii katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya safari kwenda kutoa misaada kwa wapiganaji waliopo Samara, wameandaa chakula cha aina tofauti pamoja na vifaa mbalimbali, hali kadhalika mgahawa wa maimamu wawili Askariyyani (a.s) umepewa aina mbalimbali za vyakula.

Kiongozi wa idara ya Diyala chini ya ustawi wa jamii Sayyid Hassan Mussawi amesema kuwa: “Leo tumekwenda kusaidia wapiganaji waliopo Samara kama sehemu ya kuonyesha umuhimu wao na kazi kubwa ya kulinda amani katika mji huo, kikosi cha tano cha Hashdu Shaábi kimepewa aina zote za chakula wanacho hitaji”.

Akaongeza kuwa: “Msafara huo pia umebeba aina tofauti za chakula kwa ajili ya mgahawa unaotoa huduma ya chakula kwa mazuwaru wa Imamu Ali Haadi na Hassan Askariy (a.s) tena wamepewa aina za vyakula walivyo hitaji”.

Kumbuka kuwa idara ya Diyala pamoja na mawakibu zilizo chini yake, mara nyingi wamekuwa wakiandaa vitu mbalimbali na kuvigawa kwa wapiganaji waliopo katika kambi za Samaraa takatifu pamoja na katika mgahawa wa maimamu wawili Askariyyaini (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: