Mkuu wa majeshi wa Iraq atembelea Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu na makamo wake pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya uongozi na mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, wamempokea mkuu wa majeshi ya Iraq jenerali Abdul-Amiir Rashidi Yarallah aliye ongozana na mkuu ya majeshi ya ardhini na jopo la viongozi wa wizara ya ulinzi pamoja na mkuu wa kikosi cha ulinzi cha mkoa wa Karbala, ziara hiyo imefanywa siku ya Jumatatu mwezi (6 Dhulhijjah 1441h) sawa na tarehe (27 Julai 2020m).

Ugeni huo umefanya ibada ya ziara na kusoma dua mbele ya kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s), mwishoni mwa kikao Yarallah akapongeza kazi kubwa inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika sekta ya afya, ulinzi pamoja na sekta zingine, kisha akaagwa kwa bashasha kama alivyo pokelewa.

Kumbuka kuwa ugeni rasmi hutembelea Atabatu Abbasiyya tukufu na kufanya ziara pamoja na kusoma dua kila baada ya muda fulani, halafu huangalia harakati mbalimbali zinazo fanywa na Ataba takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: