Msiba wa Imamu Baaqir (a.s): Atabatu Abbasiyya tukufu imepandisha bendera za kuashiria huzuni na kuta zake zimewekwa mapambo meusi

Maoni katika picha
Kuta za Atabatu Abbasiyya tukufu na korido zake zimewekwa mapambo meusi, kama ishara ya kuonyesha huzuni ya kifo cha Imamu wa tano Muhammad Baaqir (a.s), pia zimewekwa mabango yaliyo andikwa manone yanayo onyesha mapenzi na utiifu kwake pamoja na kuonyesha maumivu wanayo pata wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kutokana na msiba huo.

Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba kamili kuhusu maombolezo haya, yenye vipengele vichache kutokana na mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa ya kuwepo kwa maambukizi ya virusi vya Korona, sambamba na kuzingatia maelekezo ya idara ya afya yanayo kataza mikusanyiko ya watu.

Kumbuka kuwa Imamu Baaqir (a.s) alizaliwa mwezi wa Rajabu mwaka wa (57h) katika mji wa Madina na akafa kishahidi mwezi (7) Dhulhijjah mwaka wa (114h) kwa sumu, na akazikwa katika makaburi ya Baqii-Kharqad.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: