Atabatu Abbasiyya tukufu inaomboleza kifo cha Imamu Baaqir (a.s)

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu wa tano Muhammad Baaqir (a.s), kama kawaida yake katika kuomboleza vifo vya Maimamu watakasifu (a.s).

Majlisi hiyo imefanywa ndani ya ukumbi wa utawala katika Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na kuchukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona na kuhudhuriwa na watumishi wachache wa Abulfadhil Abbasi (a.s).

Mzungumzaji alikua ni Shekh Ali Mujani kutoka kitengo cha Dini, amezungumzia historia ya maisha ya Imamu Baaqir (a.s) yaliyojaa elimu, aidha ameeleza changamoto alizo pambana nazo Imamu (a.s) kutoka kwa watawala wa Umawiyya wa kipindi chake, akamaliza kwa kueleza tukio la kifo chake (a.s).

Majlisi hii ni sehemu ya muendelezo wa majlisi za kuomboleza misiba ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s) misiba iumizayo nafsi za waumini na wapenzi wa Ahlulbait (a.s). Kumbuka kuwa mwezi saba (7) Dhulhijjah ndio siku aliyokufa kishahidi Imamu Muhammad Baaqir (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: