Watumishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji wanapuliza dawa katika ofisi za wizara ya mafuta

Maoni katika picha
Wawakilishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdu-Shaábi) katika mji mkuu wa Bagdad, wameitikia wito wa wizara ya mafuta, wanapuliza dawa kwenye ofisi za wizara ya mafuta chini ya maelekezo ya kamanda mkuu wa kikosi hicho ya kupambana na janga la Korona.

Msemaji wa kikosi ameripoti kuwa: Tumefanikiwa kupuliza dawa katika ofisi za wizara pamoja na kuongezeka kwa kiwango cha joto, kazi ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona pamoja na kuwalinda wananchi dhidi ya virusi hivyo inafanyika kama kawaida.

Akaongeza kusema kuwa: kazi ya kupuliza dawa imefanywa kwa kutumia vifaa vya kisasa pamoja na dawa maalum zinazo tengenezwa na shirika la Aljuudi ambalo lipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kumbuka kuwa kikosi cha Abbasi (a.s) kiliunda kamati maalum ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, inayofanya shughuli mbalimbali za kupambana na maambukizi ya virusi hivyo, ikiwa ni pamoja na kupuliza dawa katika mji wa Karbala na miji mingine ya Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: