Mwezi tisa Dhulhijah aliuwawa balozi wa harakati ya Husseiniyya na shahidi wa kwanza wa harakati hiyo Muslim bun Aqiil (a.s)

Maoni katika picha
Katika siku kama ya leo mwezi tisa Dhulhijah mwaka wa 60 hijiriyya, aliuwawa kikatili balozi wa Imamu Hussein bun Ali bun Abu Twalib (a.s), aliyeteuliwa na Imamu (a.s) kuwa balozi wake kwa watu wa Kufa, baada ya kupokea barua nyingi kutoka kwa watu hao wakimuomba aende kuwaokoa na dhulma za utawala wa Umawiyya.

Imamu (a.s) akaona ni vizuri amteue balozi atakaekwenda kuangalia ukweli wao, akikuta kama ni wakweli achukue kiapo cha utii kisha Imamu ndio aende kwao, akamteua mtu anayemuamini zaidi na mkubwa kwa umri katika watu wa familia yake Muslim bun Aqiil, mtu mwenye uwezo mkubwa wa kupambana na mazingira magumu na mwenye msimamo imara kwenye matatizo, Imamu (a.s) akamuambia achukue jukumu hilo, naye alikubali kwa furaha na bashasha, akampa barua iliyokua inaeleza utukufu wa Muslim (a.s).

Imepokewa kuwa kiongozi wa waumini (a.s) alimuambia Mtume (s.a.w.w): Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hakika wewe unampenda Aqiil? Mtume (s.a.w.w) akasema, ndio! Wallahi nampenda mara mbili, nampenda yeye na ninampenda kwa mapenzi ya Abu Twalib kwake, na mtoto wake atauliwa kwa ajili ya kumpenda mtoto wako, ataliliwa na waumini na ataombewa rehema na malaika, kisha Mtume (s.a.w.w) akalia hadi machozi yakalowesha kifua chake, halafu akasema: Namshitakia Mwenyezi Mungu kwa mitihani watakayopata kizazi changu baada yangu. (Amali Swaduuq, ukurasa wa 111).

Hatakama tusingepokea hadithi yeyote kuhusu utukufu wa Muslim hii ingetosha kuonyesha utukufu wake, Mtume anaeleza kifo chake na kulia pamoja na kusema kuwa waumini watamlilia, jambo hilo linaonyesha ukubwa wa hadhi yake.

Miongoni mwa yanayo onyesha hadhi yake ni barua iliyo andikwa na bwana wa mashahidi alipomtuma kwenda Kufa; alisema (a.s): “Nakutumieni ndugu yangu na mtoto wa Ammi yangu muaminifu zaidi kwangu katika watu wa nyumba yangu Muslim bun Aqiil”. (Biharu-Anwaar juzu la 44, ukurasa wa 334), kuchaguliwa Muslim kama balozi wa harakati ya Imamu Hussein kunaonyesha ukubwa wa nafasi yake pamoja na jinsi Imamu Hussein anavyo muamini na heshima aliyo nayo kwa watu wa Kufa, ndio maana akamsifu kwa kusema kuwa ni muaminifu katika watu wa nyumba yake.

Muslim alipo fika Kufa watu walimpokea kwa shangwe na furaha, akawasomea barua ya Abu Abdillahi Hussein (a.s), akawaambia kuwa yuko tayali kuja kwao kama watatoa kiapo cha utii na wakaonyesha subira katika kupambana na maadui zao, baada ya kuwaambia kuwa anataka wale kiapo cha utii, watu walimiminika kwake na kula kiapo cha utii, huku wakisema kuwa wameridhia na wako tayali, Muslim akamuandikia Hussein habari hiyo na akamtaka aje haraka, lakini watu hao walibadilika haraka sana, yakamletea Muslim madhila makubwa baada ya watu hao kuvunja ahadi zao na viapo vyao.

Ibun Ziyadi alitoa amri ya kufanya upekuzi katika nyumba zote za Kufa, kwa ajili ya kumtafuta Muslim bun Aqiil (a.s), aliyekua amejificha kwenye nyumba ya mwanamke mpenzi wa watu wa nyumba ya Mtume (a.s), mwanamke huyo anaitwa (Twauá), Ibun Ziyadi alipojua sehemu alipo alituma jeshi kwenda kumkamata, Muslim alipigana vita kali sana hawakuweza kumkamata kwa urahisi, hadi walipo tumia njama na udanganyifu ndio wakafanikiwa kumkamata na kumpeleka kwenye Qasri, ndipo Ibun Ziyadi akaamuru apelekwe juu ya Qasri na auwawe kisha mwili wake utupwe chichi, Muslim akakatwa kichwa na kutenganishwa na mwili wake, ikawa ni tiketi ya kumkutanisha na mashahidi, wakweli, manabii waja wema na hao ndio marafiki bora.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: