Muhimu: Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kuwa haitaswali Idul-Adh-ha

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umetangaza kuwa hakutakuwa na swala ya Idul-Adh-ha, kutokana na mazingira ya kiafya ambayo taifa la Iraq linapitia kwa sasa.

Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Abbasi Mussawi Ahmadi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kutokana na malekezo yaliyo tolewa na idara ya afya ya mkoa wa Karbala na katika kufanyia kazi maelekezo hayo, tumekubaliana kutokuwepo kwa swala ya Idul-Adh-ha tukufu ya mwaka huu 1441h”.

Akabainisha kuwa: “Maamuzi haya yametokana na mazingira ya afya yaliyopo hivi sasa pamoja na maelekezo yaliyo tolewa na idara ya afya ya mkoa wa Karbala yaliyo zuwia mikusanyiko mikubwa ya watu”.

Kumbuka kuwa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya mwezi (15 Rajabu 1441h) sawa na (11 Machi 2020m) zilitoa tamko la kusimamisha swala za jamaa kama sehemu ya kufanyia kazi maelekezo ya idara ya afya ya Karbala na kulinda usalama wa mazuwaru watukufu.

Tambua kuwa Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani alijibu swali lililotumwa katika ofisi yake linalo husu hukumu ya kushiriki swala ya jamaa katika mazingira ya kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Korona.

Swali lilikuwa linasema: Ni upi mtazamo wa Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu kuhusu kushiriki swala ya jamaa katika siku hizi ambazo tunashuhudia muenea kwa maambukizi ya virusi vya Korona?

Jawabu: Kwa kuwa mikusanyiko ya watu imekatazwa kwa lengo la kujikinga na kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Korona, inafaa kuzingatia katazo hilo na kulifanyia kazi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: