Muhimu: maelekezo ya ofisi ya Marjaa Dini mkuu kuhusu maombolezo ya Ashula

Maoni katika picha
Ofisi ya Marjaa Dini mkuu leo siku ya Alkhamisi mwezi (9 Dhulhijjah 1441h) sawa na tarehe (30 Julai 2020m) imejibu swali kuhusu kufanya maombolezo ya Imamu Hussein (a.s) katika mwezi wa Muharam mwaka 1442h.

Ifuatayo ni nakala ya maelezo hayo iliyo wekwa kwenye mtandao wa Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Ayatullahi Sayyid Sistani (udumu utukufu wake):

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu

Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Sayyid Sistani

Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yako na rehema pamoja na baraka zake.

Amma baada:

Kutokana na kukaribia mwezi mtukufu wa Muharam, mwezi wa kuomboleza msiba wa Twafu, sambamba na kuendelea kwa maambukizi ya virusi vya Korona, na kuendelea kusisitizwa ulazima wa kujiepusha na mikusanyiko mikubwa hususan katika maeneo ya ndani, watu wengi wanauliza cha kufanya wakati wa kuomboleza kifo cha bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake (a.s), pamoja na shauku kubwa waliyo nayo ya kuomboleza msiba huo kama walivyo zowea, tunaomba ufafanuzi wa hilo na tunatanguliza shukrani nyingi kwenu.

Kundi la waumini wa Najafu Ashafu

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu

Amani iwejuu ya Hussein na watoto wa Hussein na wafuasi wa Hussein na rehema za Mwenyezi Mungu na baraka zake.

Hakika kuna njia nyingi za kuonyesha huzuni na majonzi katika msiba huu mkubwa, na kumpa pole Mtume (s.a.w.w) pamoja na watu wa nyumbani kwake kwenye msiba huo mkubwa katika uislamu na waislamu, miongoni mwa njia hizo ni:

  • 1- Kurusha matangazo mubashara ya kuomboleza kwenye luninga na mitandao ya intanet, vituo na taasisi za Dini ziwasiliane na wahadhiri wazuri pamoja na waimbaji wa kaswida za kuomboleza kwa ajili ya kuwarekodi na kuwarusha kwenye luninga na mitandao ya intanet, na watu wahimizwe kufuatilia mihadhara hiyo wakiwa majumbani kwao.
  • 2- Kufanya majlisi za nyumbani kwa muda mfupi usiku au mchana, na kuhudhuriwa na wanafamilia na watu wa karibu yao, na kusikiliza mihadhara kwenye luninga au kwenye mitandao ya intanet, majlisi za kuhusisha watu wengi lazima zifuate taratibu za afya zilizo wekwa na idara husika, watu wakae kwa umbali unao takiwa na wavae barakoa sambamba na kuchukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, pamoja na kuhudhuriwa na watu wachache kulingana na sehemu inapo fanyika majlisi hiyo kama ni sehemu ya wazi au ndani, pamoja na kutofautiana kwa mazingra ya nchi kuhusu maambukizi ya virusi vya Korona.
  • 3- Kuweka mabango na ishara za maombolezo ya Ashura kwa kupandisha bendera nyeusi, kufunga vitambaa vyeusi kwenye viwanja, barabara na sehemu za umma, sambamba na kuheshimu haki za wamiliki wa maeneo ya watu binafsi na kutii sheria za nchi, sambamba na kuandika ujumbe wa Imamu Hussein (a.s) aliotoa katika harakati yake ya Islahi, kuhusu chakula ambacho watu wamezowea kugawa katika maombolezo hayo lazima zichukuliwe tahadhari za kiafya katika uandaaji na ugawaji wake, hata kama ikibidi kutosheka na kugawa chakula kibichi katika nyumba za waumini ili kuepusha misongamano.

Mwenyezi Mungu awawezeshe nyote kuomboleza msiba huu muhimu wa bwana wa mashahidi wa peponi (a.s) kulingana na mazingira ya sasa, hakika yeye ni mkuu wa taufiq.

9 Dhulhijjah 1441h

Ofisi ya Sayyid Sistani (udumu utukufu wake) – Najafu Ashrafu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: