Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu unatoa mkono wa pongezi kwa Imamu wa zama Mahadi msubiriwa (a.f), na Maraajií watukufu pamoja na waislamu wote duniani, kwa kuingia sikukuu tukufu ya Idul-Adh-ha, Mwenyezi Mungu ajaalie amani na afya, tunamuomba Mwenyezi Mungu alipe taifa letu amani na utulivu, na aondoe mabalaa na kuwaponya haraka wagonjwa pamoja na kukubali maombi ya waumini wote pamoja na ibada zao, Allah akupeni kheri nyingi na baraka.