Kusafisha na kupuliza marashi katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Watumishi wa idara ya usimamizi wa haram katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wanasafisha na kupuliza marashi kwenye haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ikiwa ni pamoja na eneo linalozunguka dirisha la kaburi na kwenye korido zote.

Kiongozi wa idara hiyo bwana Nizaar Ghani ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kazi yetu inaendelea ndani ya haram tukufu kwa kufuata ratiba maalum, kuna baadhi ya mambo yameongezwa kutokana na kuwepo kwa maambukizi ya virusi vya Korona, kazi ya usafi inachukua muda mferu, tunasafisha eneo lote la haram takatifu”.

Akaongeza kuwa: “Tumesafisha na kupuliza marashi wenye dirisha takatifu kwa kutumia vifaa maalum pamoja na kupuliza dawa, kisha tukaelekea sehemu zinazo zunguka haram hadi kwenye korido zake nne, tumesafisha sehemu yote ya chini na kuta zake pamoja na kupuliza dawa, ili kulinda usalama wake na kuondoa bakteria wanaoweza kusababisha maradhi kwa mazuwaru watukufu, tumetumia vifaa maalum vya usafi na dawa za kuuwa bakteria, pamoja na kupuliza marashi”.

Akamaliza kwa kusema: “Baada ya kumaliza kuosha kama kawaida tumepuliza marashi mazuri, kwenye dirisha la kaburi na sehemu zingine zote hadi kwenye marumaru”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: