Kituo cha utamaduni wa familia kinaendesha shindano la bibi Sara (a.s) kwa njia ya mtandao

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetangaza shindano la bibi Sara (a.s) litakalo fanyika kwa njia ya mtandao, kufuatia kuingia kwa sikukuu ya Idul-Adh-ha, litafanyika katika siku zote za sikukuu kwa wanawake tu, shindano hili ni muendelezo wa mashindano mengine yaliyo fanywa siku za nyuma, linalenga kuwajenga kiutamaduni wakina mama na kuongeza maarifa yao.

Mkuu wa kituo hicho bibi Asmahani Ibrahim amesema kuwa: “Shindano hili ni sehemu ya mashindano mengi yanayo simamiwa na kituo katika kipindi hiki cha maambukizi ya virusi vya Korona, kama sehemu ya kutumia muda viruri kwa wakina mama, shindano hili tumeliita bibi Sara (a.s) linamaswali kadhaa, mada kuu ni ibada ya Hijja na hukumu zake, pamoja na maswali ya kihistoria kuhusu swala hilo”.

Akafafanua kuwa: Utashiriki kwa kutumia linki ifuatayo: https://forms.gle/W4gRLaUmDx8RHuhP8

Kutakuwa na washindi wanne baada ya kuwapigia kura wale watakao jibu sahihi.

Kwa maelezo zaidi angalia mitandao ifuatayo:

https://t.me/thaqafaasria1

instagram: (thaqafa_ausaria)

telegram: (https://t.me/thaqafaasria1)

facebook: : (https://www.facebook.com/thaqafaasria1).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: