Mawakibu za kutoa misaada kutoka mikoa mitatu zimekuja kusaidia kituo cha kuoshea maiti cha Yaasiin

Maoni katika picha
Mawakibu za kutoa misaada zilizo chini ya idara ya ustawi wa jamii katika Atabatu Abbasiyya tukufu zimetoa vifaa vya lazima katika kituo cha Yaasiin, ambacho kipo chini ya kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, (Liwaau/26 Hashdu Shaábi), vinavyo hitajika katika kuosha na kumvisha sanda mtu aliyekufa kwa ugonjwa wa Korona, kilicho jengwa siku chache zilizo pita.

Idara zilizo shiriki katika kutoa vifaa hivyo zimetoka kwenye mikoa mitatu, ambayo ni Bagdad/ Raswafa, Misaan na Diyala.

Kwa mujibu wa bwana Swafa Sudani kiongozi wa idara ya Misaan, amesema kuwa: “Leo tumewasili Karbala tukiwa na mawakibu zetu kutoka Misaan, kwa lengo la kutoa misaada kwenye kituo cha Yaasiin ambacho kipo chini ya kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, vinavyo hitajika katika kuosha na kuvisha sanda watu waliokufa kwa ugonjwa wa Korona, tutakuja tena kama ikilazimika hivyo –Allah atuepushie-“.

Nae bwana Muhammad Ghazawi kiongozi wa idara ya Bagdad/ Raswafa amesema kuwa: “Kutokana na maelekezo ya moja kwa moja kutoka kwa kiongozi wa idara ya ustawi wa jamii katika Atabatu Abbasiyya tukufu, tumeamua kuja kutoa vitu vinavyo hitajika katika kituo cha Yaasiin hapa Karbala, msaada wetu haukuishia kwenye kituo hicho peke yake, bali tumesaidia pia kituo cha Liwaau/2 Hashdu Shaábi kilicho chini ya kikosi cha Imamu Alli (a.s) katika mkoa wa Najafu”.

Sayyid Hassan Mussawi kiongozi wa mawakibu za Diyala amesema kuwa: “Kutoa msaada huu ni sehemu ya wajibu wetu kibinaadamu, ambao umekuwa ukitekelezwa na mawakibu zetu tangu lilipotokea janga hili hapa nchini, yatupasa kusimama pamoja na ndugu zetu wanaojitolea kufanya kazi hii kwa kuwapa vitendeakazi muhimu”.

Kumbuka kuwa idara ya ustawi wa jamii iliagiza matawi yake yote kusaidia shughuli zinazofanywa na Atabatu Abbasiyya kwenye sekta ya afya hapa nchini na kusaidia waathirika wa janga la Korona, sambamba na kusaidia watumishi wa afya wanao pambana na janga la Korona, kama vile kuwapa mashine za kupumlia, dawa za kupuliza barakoa na vinginevyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: