Tambua utendaji wa kazi katika kituo cha kuosha maiti waliokufa kwa janga la Korona cha “Yaasiin”

Maoni katika picha
Watumishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdu Shaábi) wanaendelea na kazi katika kituo cha kuosha maiti za watu waliokufa kwa janga la Korona cha “Yaasiin”.

Kiongozi wa kituo hicho Ahmad Ni’mah amesema kuwa: “Kituo kinawatumishi wanaume na wanawake kwa ajili ya shughuli za kuosha na kuvisha sanda”.

Akabainisha kuwa: “Asilimia kubwa ya waoshaji ni majemedari waliojitolea kuitikia wito wa Marjaa wa kupambana na kundi la magaidi la Daesh, aidha kuna wakina mama waliojitolea kutoka mikoa tofauti”.

Akaongeza kuwa: “Huduma zote za kumuandaa maiti na kumzika zinatolewa bure, gharama zote zimefadhiliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu”, akasema: “Kama mfiwa anamiliki sehemu yake binafsi ya kuzikia, marehemu wake anaweza kuzikwa sehemu hiyo chini ya usaidizi wa wahudumu wa kikosi cha Abbasi, kama hana sehemu basi marehemu wake atazikwa kwenye makaburi baalum yaliyo pangwa na serikali “.

Mjumbe wa kamati inayo simamia shughuli za mazishi bwana Ali Abdurahim Ahmad amesema kuwa: “Watu wanaofanya kazi kwenye kituo hiki wanaushirikiano mkubwa kama nyuki, wanaanza kazi saa tatu (3) asubuhi hadi saa kumi na mbili (12) jioni, muda huo wa mcha huandaa vitu vinavyo hitajika kwenye shughuli ya mazishi na mazishi huanza jioni hadi saa nane (8) usiku”. Akasema kuwa: “Upokeaji wa maiti hufanywa kwa kushirikiana na idara ya afya ya Karbala au ya mkoa inakotoka maiti, kwani huandikwa taarifa nzima ya kifo cha marehemu na kuthibitishwa na pande zote mbili, upande wa idara inayo kabidhi na upande wa wahudumu wa shughuli za mazishi, upande wa pili unahusisha wasomi wa Dini kwa ajili ya kusimamia shughuli za kuandaa maiti hadi kuzika, hufanya hadi mambo ya sunna kama vile ziara talqini na mengineyo”.

Watu wanaojitolea kufanya kazi hii wanatoka mikoa yote na wanafanya kazi katika mazingira magumu, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu atuondolee haraka balaa hili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: