Kitengo cha malezi na elimu ya juu kinatafuta njia ya kupanua ufundishaji kwa njia ya mtandao mashuleni

Maoni katika picha
Katika mkakati wa maendeleo unaofanywa na kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, hususan mambo yanayo husu kutumia teknolojia ya kisasa katika ufundishaji, kitengo cha mahusiano kinaboresha ufundishaji kwa njia ya mtandao katika shule za Al-Ameed.

Wamefanya kikao cha kujadili njia za ufundishaji kwa kutumia mitandao, kilicho hudhuriwa na jopo la walimu waliobobea katika fani hiyo, wamejadili na kuweka mikakati ya utekelezaji wa mradi huo katika shule za Al-Ameed, ukizingatia kuwa tunaishi katika mazingira ya maambuizi ya virusi vya Korona, kwani janga hili linaweza kuendelea hadi mwaka ujao wa masomo.

Mjumbe wa kamati ya ufundishaji kwa njia ya mtandao Dokta Hassan Jadhili amesema kuwa: “Ufundishaji wa kutumia mitandao unahitaji uwepo wa mwalimu na mwanafunzi kwenye mtandao kwa wakati mmoja, pia inawezekana mwalimu na mwanafunzi wasiwe kwenye mtandao kwa wakati mmoja, njia hiyo mwalimu atatuma masomo kwenye mtandao kwa njia rahisi ambayo wakati wowote mwanafunzi akiingia kwenye mtandao anaweza kujisomea na kuelewa somo kwa urahisi”.

Akasema: “Warsha hiyo itaendelea kwa muda wa siku (15) kwa muda wa saa nne za masomo kila siku”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: