Kukamilika hatua ya kwanza ya matengenezo katika hospitali ya watoto ya Karbala

Maoni katika picha
Pamoja na kufanya ujenzi wa nje kama vile vituo vya Alhayaat kwa ajili ya kuhudumia watu walioambukizwa virusi vya Korona katika mikoa tofauti, na kazi za ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi wamekamilisha hatua ya kwanza katika matengenezo ya baadhi za sehemu ya hospitali ya watoto mjini Karbala, na wameanza hatua ya pili.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mhandisi Muhammad Mustwafa Twawil kiongozi wa idara ya ujenzi huo amesema kuwa: “Tumetengeneza vyoo vya hospitali vilivyo kuwa vimeharibika, eneo la vyoo linaukubwa wa mita (18) na kuna vyoo sita pamoja na sehemu ya kuoshea mikono”.

Akaongeza kuwa: “Ujenzi wa vyoo hivyo umekamilika na ulipitia hatua tofauti, tuliondoa sakafu ya zamani na kuijenga upya pamoja na kuta zake, hali kadhalika tumejenga upya dari lake na kuweka feni za kutoa hewa chafu pamoja na kufunga mota za kuchemsha maji, tumeweka milango mipya na tumerudia upya kuweka mfumo wa maji na tumeweka viti vipya”.

Akabainisha kuwa: “Tunaendelea na hatua ya pili itakayo husisha majengo mawili ya vyoo na kurekebisha njia za eneo la Hoapitali”.

Kumbuka kuwa kazi ya kukarabati baadhi ya maeneo katika hospitali hii ni sehemu ya miradi ya kibinaadamu inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, na inayolenga kukarabati baadhi ya majengo ya hospitali yaliyo haribika, kama vile majengo ya shule, taasisi za kibinaadamu na mengineyo.

Idara ya hospitali imeshukuru Atabatu Abbasiyya tukufu na watendaji wa mradi huo, imesema kuwa sio jambo geni kwa Ataba kufanya miradi ya aina hii hususan katika mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa ya kuenea kwa maambukizi ya viruri vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: