Kwa mnasaba wa Idul-Ghadiir: idara ya Qur’ani inafanya shindano maalum kwa ajili wa wanawake tu liitwalo (Mnara wa Dini)

Maoni katika picha
Idara ya Qur’ani chini ya ofisi ya maelekezo ya Dini kitengo cha wanawake kinacho fungamana na ofisi ya katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya wanafanya shindano maalum kwa wanawake tu kupitia njia ya mtandao, liitwalo (Mnara wa Dini).

Kiongozi wa idara hiyo Ustadhat Fatuma Sayyid Abbasi Mussawi amesema kuwa: “Shindano hili ni sehemu ya kuadhimisha Idul-Ghadiir, na kuenzi utamaduni wa Qur’ani na Aqida, ili tukio la Ghadiir liendelee kuishi katika jamii yetu na kuadhimishwa kila mwaka, kwani tukio hilo ni katika misingi ya Dini inayo dumisha ujumbe wa mbora wa Mitume (s.a.w.w).

Akafafanua kuwa: Masharti ya shindano hili ni:

  1. Mshiriki lazima awe mwanamke.
  2. Mshiriki asiwe na umri chini ya miaka 17.
  3. Aandike majina yake manne atakaye halifu jibu lake halitazingatiwa.
  4. Hairuhusiwa kushiriki shindano zaidi ya mara moja.
  5. Mshiriki aandike namba yake ya simu.

Siku ya mwisho ya kushiriki ni Ijumaa (Agosti 7), majina ya washindi yatatangazwa baada ya kupiga kura siku ya Jumamosi (siku ya Idul-Ghadiir) na zawadi za washindi zipo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: