Kutokana na sikukuu ya Idul-Ghadiir shule za Alkafeel za wasichana zimetangaza shindano kwa wanawake tu

Maoni katika picha
Kutokana na kukaribia kwa Idul-Ghadiir idara ya shule za Alkafeel za wasichana chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza shindano la utafiti wa uhusiano wa siku ya Ghadiir na wilaya ya Imamu wa kumi na mbili Hujjat bun Hassan (a.s) kwa wasichana tu.

Kiongozi wa idara hiyo bibi Bushra Kinani ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kuwa: “Shindano hili linaangazia tukio tukufu na kuliowanisha na Imamu Hujjat (a.f), hakika siku ya Ghadiir ni siku ya ahadi na kutangaza ukuu wa Mwenyezi Mungu na kula kiapo cha utii, Mahadi (a.f) ndio Imamu wa mwisho, swali linasema: Kuna uhusiano gani kati ya siku ya Ghadiir na uongozi wa Imamu wa kumi na mbili (a.f)?

Akafafanua kuwa: “Tarehe ya mwisho kupokea majibu itakuwa siku ya Jumatatu (10 Agosti 2020m) saa kumi jioni, jibu linatakiwa kukamilisha masharti yafuatayo:

  • - Hatutaki utafiti uliochukuliwa kutoka kwenye mitandao ya kielektonik (intanet).
  • - Jibu liendane na maudhui inayo kusudiwa na swali.
  • - Jibu lisizidi maneno (8000) na yeyote atakae zidisha maneno hayo jibu lake halitazingatiwa.
  • - Uandike muhtasari wa jibu na kuutuma, baada ya muhtasari kupasishwa ndio unatuma jibu lote.
  • - Washindi watatu wa kwanza watapewa zawadi kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu.
  • - Kila mshiriki atapewa cheti cha ushiriki kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: