Kikosi cha Abbasi cha wapiganaji kinaendelea kupambana na janga laKorona

Maoni katika picha
Wawakilishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdu Sha’abi) wanaendelea kupambana na janga la Korona kwenye mikoa tofauti, baada ya kupokea wito kutoka kwa wakazi wa mji wa Bashiri kitongoji cha Lailani, wawakilishi wamekwenda kutoa matibabi na kusaidia vifaa vya oksijen kwa wagonjwa waliohamishwa majumbani mwao sambamba na kutoa huduma hizo katika mji wa Diwaniyya.

Msemaji wa kikosi ameripoti kuwa: Kikosi cha majibu ya haraka chini ya idara ya mawasiliano ya kikosi cha Abbasi (a.s) katika mji wa Bashiri, kimekwenda kutoa huduma ya matibabu na vifaa vya kupumlia Oksijen kwa wahitaji wa kitongoji cha Lailani, kuhusu kazi inayo endelea katika mkoa wa Waasit, amesema kuwa: wahudumu wetu wa Diwaniyya wanaendelea kupuliza dawa katika nyumba za mji huo, hususan kwenye maeneo ambayo yameripoti visa vya maambukizi, wakazi wa maeneo hayo wameshukuru sana msaada huo.

Kumbuka kuwa kikosi kiliunda kamati maalum ya kupambana na janga la Korona, kamati hiyo imesha puliza dawa sehemu mbalimbali za makazi ya watu, ndani na nje ya mji wa Karbala, inafanya kila iwezalo katika kupambana na janga hili, hivi karibuni imejenga kituo maalum kwa ajili ya kuosha na kuzika watu watakaokufa kwa janga la Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: