Kituo cha utamaduni wa familia kinafanya shindano la Idul-Ghadiir kwa wanawake na kimeandaa zawadi za washindi

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kuanza kwa shindano la Idul-Ghadiir chini ya kauli mbiu isemayo (Kueneza furaha za Ghadiir ni kilele cha shangwe ya sikukuu) kwa ajili ya kuhuisha na kukumbuka siku ya wilaya na baiyya Idi kubwa ya Mwenyezi Mungu, shindano hili linasaidia kuongeza uwelewa wa tukio hilo kwa wanawake na kituo kimetoa wito kwao wa kushiriki aidha zawadi za washindi tayali zimesha andaliwa.

Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa kituo hicho Ustadhat Asmahani Ibrahim amesema kuwa: “Hili ni moja ya mashindano mengi yanayo fanywa na kituo chetu kwenye matukio mbalimbali ya kidini, tumeandaa ratiba kamili ya mashindano hayo, likiwemo tukio hili muhimu, tukio la kuvishwa taji kwa kiongozi wa waumini Ali (a.s) taji la usia na wilaya”.

Akaongeza kuwa: “Shindano linamaswali ishirini (20) yaliyo andaliwa na kamati maalum, yanahusu malengo ya mnasaba huu, pamoja na baadhi ya maswali yanayo muhusu muadhimishwa (a.s), shindano hili litadumu kwa siku nne”.

Akasema kuwa: “Shiriki shindano kupitia link ifuatayo: (https://forms.gle/W4gRLaUmDx8RHuhP8), majibu sahihi yatapigiwa kura na kupata washindi nane, zawadi zao tayali zimesha andaliwa, washindi watatangazwa baada ya kumaliza kusahihisha”.

Kwa maelezo zaidi angamia mtandao ufuatayo:

https://t.me/thaqafaasria1
au telegram: (thaqafa_ausaria)

na facebuuk: (https://www.facebook.com/thaqafaasria1).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: