Dirisha la kaburi la mtoto wa mwenye kupewa baiyya Abulfadhil Abbasi (a.s) limepambwa mauwa

Maoni katika picha
Katika kujiandaa na Idi kubwa ya Mwenyezi Mungu Idul-Ghadiir ambayo kumbukumbu yake inasadifu siku ya Jumamosi mwezi (18 Dhulhijjah 1441h) sawa na tarehe (8 Agosti 2020m), dirisha la mtoto wa aliyepewa baiyya katika bonde la Ghadiir Abulfadhil Abbasi (a.s) limewekwa mauwa na marashi kama sehemu ya kuonyesha furaha kufuatia tukio hilo tukufu ambalo huchukuliwa kuwa sikukuu kubwa kwa waislamu.

Mauwa hayo yamewekwa na wahudumu wa idara ya miti na mapambo chini ya kikundi cha vitalu vya Alkafeel, kwa kufuata utaratibu maalum wa kanuni za kujikinga na maambukizi.

Masayyid wachache ndio walibeba mauwa na kuyaweka juu ya dirisha la kaburi, wakianza kwa kufanya ziara kwenye malalo takatifu na kusomea dua waislamu wote na wapenzi wa Ahlulbait (a.s) awape afya na amani, na awaondolee balaa hili kwa baraka za mwenye maadhimisho haya.

Mauwa hayo sio kwamba yamewekwa kwenye malalo takatifu tu, bali yamewekwa hadi nje ya malalo, kwenye milango, korido na kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili takatifu ambao unameremeta kwa mauwa na mapambo.

Kumbuka kuwa kwa ajili ya kuzingatia maelekezo ya kujikinga na maambukizi, yaliyo tolewa na idara ya afya ya Karbala pamoja na maagizo ya Marjaa Dini mkuu, Atabatu Abbasiyya tukufu imekusudia kutofanya shughuli yeyote kufuatia maadhimisho haya kutokana na mazingira ya afya ambayo Iraq inapitia kwa sasa na dunia kwa ujumla.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: