Kituo cha turathi za Basra kimechapisha kitabu cha (Uhai wa siasa za Basra)

Maoni katika picha
Hivi karibuni kituo cha turathi za Basra chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya kimetoa kitabu cha (Uhai wa siasa katika mji wa Basra) kuanzia mwaka wa (14h hadi 132h) sawa na (634m hadi 749m).

Kitabu hicho ni sehemu ya mausua ya turathi za Basra/ inayo elezea historia ya turathi kina kurasa (730), kimeandikwa na Dokta Hussein Lami na kuhakikiwa pamoja na kuwekwa faharasi na wasomi wa kituo.

Kitabu kimeandika wakati mgumu katika historia ya mji wa Basra, uliojaa vita na vurugu, wakati mbaya zaidi ukiwa ni ule ambao bani Umayya walitawala mji huo na kufanya jinai mbaya sana, waliasisi dhulma na kuieneza kila sehemu, kitabu kimeandika mambo mengi ya kihistoria yaliyo tokea katika mji wa Basra.

Ukitaka kusoma kitabu hicho na vingine vilivyo chapishwa na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu ingia katika toghuti ifuatayo: www.mk.iq.

Kumbuka kuwa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu ni moja ya vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu, kinajihusisha na utambuzi wa utamaduni na turathi katika jamii, sambamba na kufundisha fikra za Ahlulbait (a.s) kupitia idara na vituo vyake, miongo vya idara zake ni Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake na kituo cha turathi za Karbala, kituo cha turathi za Hilla, kituo cha turathi za Basra, shule za Alkafeel na idara ya habari na maarifa, lengo kuu ni kufundisha mambo mbalimbali katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: