Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya unatoa mkono wa pongezi kwa Imamu wa zama Mahadi msubiriwa (a.f) na Maraajii watukufu pamoja na waislamu wote kutokana na Idul-Ghadiir, Idi kubwa ya Mwenyezi Mungu, siku ya kutimia neema na kukamilika Dini na kutangazwa uongozi wa Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s), tunamuomba Mwenyezi Mungu atujaalie kuwa miongoni mwa watu wanaoshikamana na uongozi wake, na atujaalie kuwa pamoja na kiongozi wa waumini (a.s), arudishe siku hii kwa waislamu wote wakiwa katika afya nzuli na amani, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu aliruzuku taifa letu amani na utulivu, na atuondolee balaa na magonjwa, awaponye haraka wagonjwa.