Namna gani Atabatu Abbasiyya tukufu ilivyo sherehekea Idul-Ghadiir katika mazingira ya maambukizi ya virusi vya Korona

Maoni katika picha
Idul-Ghadiir ni katika matukio muhimu ambayo huadhinishwa na Atabatu Abbasiyya, ni siku ambayo alitangazwa kiongozi wa waumini (a.s) kuwa walii, wasii na khalifa wa waislamu, tukio hilo likawa sababu ya kutimia neema na kukamilika Dini, lakini katika mazingira haya ambayo taifa linapitia ya maambukizi ya virusi vya Korona na changamoto zake, sambamba na kufanyia kazi maelekezo yanayo tolewa na idara ya afya ya ulazima wa kuepuka mikusanyiko, pamoja na muongozo wa Marjaa Dini mkuu, maadhimisho ya mwaka huu tumefanya mambo machache.

Miongoni mwa mambo yaliyofanywa na Atabatu Abbasiyya katika kuadhimisha sikukuu hiyo ni:

  • - Kufungua mlango wa ziara kwaniaba na kuhuisha bai’a kwa kiongozi wa waumini (a.s) kwenye malalo yake takatifu, kupitia dirisha la ziara kwaniaba la mtandao wa kimataifa Alkafeel.
  • - Kupamba haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kuta zake zimewekwa vitambaa na mabango yaliyo andikwa maneno ya bai’a na utiifu kwa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s).
  • - Kupamba dirisha tukufu la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kuweka mauwa na kufuata kanuni zote za kujikinga na maambukizi, kazi hiyo imefanywa na jopo la masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
  • - Kituo cha taaluma na uzalishaji Alkafeel chini ya kitengo cha habari kimerusha vipande vya video kupitia mitandao yake na kwenye mtandao wa Alkafeel sambamba na matangazo mubashara ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
  • - Wamerusha program ya (Idul-Ghadiir bai’atu lilahi wa lirasuulihi), iliyo andaliwa na kitengo cha habari kwa kushirikiana na kitengo cha Dini ikiwa na sehemu kumi, ilianza siku mbili za nyuma na inaendelea baada ya siku ya Idhul-Ghadiir, ikiongozwa na Shekh Haidari Aaridhwi kutoka kitengo cha Dini, program hiyo ni mihadhara ya kitafiti kuhusu uimamu na masharti yake kwa mujibu wa mitazamo ya makundi yote ya kiislamu, anatoa mtazamo wa kila kundhi na dalili zao kutoka kwa wanachuoni wao mashuhuri, pamoja na kubainisha mtazamo sahihi kwa ushahidi wa Quráni na hadithi za Mtume na Ahlulbait (a.s).
  • - Idhaa ya Alkafeel ya muislamu wakike imeandaa vipindi maalum vya redio kwa ajili ya kuadhimisha na kuelezea tukio hilo.
  • - Kufanya mashindano mbalimbali yanayo husu kuhuisha tukio hilo, yanayo lenga kuongeza maarifa kwa washiriki kuhusu tukio hilo na historia kwa ujumla pamoja na aqida.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: