Kufuatia maadhimisho ya sikukuu kubwa ya Mwenyezi Mungu Idul-Ghadiir, Atabatu Abbasiyya tukufu imefungua mradi wa upanuzi wa mlango wa Kibla katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ndani na uwekwaji wa nakshi za mapambo ya kiislamu, sambamba na mradi wa ukarabati na uwekaji wa dhahabu kwenye kuta za pambo kubwa la dhahabu linalojulikana kwa jina la (sega), shughuli za ufunguzi huo zimefanywa alasiri ya leo mwezi (18 Dhulhijjah 1441h) sawa na tarehe (8 Agosti 2020m) na kuhudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, pamoja na katibu mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar na makamo wake pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya uongozi bila kumsahau mkuu wa mkoa wa Karbala Mhandisi Naswifu Jaasim Khatwabi.
Shughuli za tukio hilo zilifunguliwa kwa Quráni tukufu, ikafuata kaswida iliyosomwa na kiongozi wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Adnani Mussawi, beti zake zilizungumzia mafanikio hayo mawili, kisha wahudhuriaji wakaelekea kwenye ufunguzi wa mradi wa kwanza, ambao ni upanuzi wa mlango wa Kibla katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ndani na uwekwaji wa nakshi na mapambo ya kiislamu.
Baada ya hapo wakaenda kufungua mradi wa pili ambao ni uwekaji wa dhahabu kwenye ukuta wenye pambo kubwa la dhahabu linalojulikana kwa jina la (sega).
Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh amesema kuwa: “Kukamilika kwa miradi hii miwili katika mazingira haya ni mafanikio makubwa yanayo ingizwa kwenye mafanikio mengine yaliyo tangulia, pia ni sehemu ya kuonyesha uwezo wa raia wa Iraq katika kufanya miradi ya aina hii, miradi hii inavionjo vya ufundi wa zamani na wa sasa, imefanywa kwa ubora wa hali ya juu kabisa chini ya mafundi mahiri walioazimia kuboreha mlango huu mtukufu unao elekea kwenye haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Mkuu wa shirika lililo tekeleza miradi hiyo Mhandisi Hamidi Majidi amesema kuwa: “Mlango wa Kibla katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) umekuwa bora zaidi kushinda milango mingine yote ya Ataba tukufu, pamoja na wingi wa mapambo yake lalini yanamuingiliano mzuri, kuhusu uwekaji wa dhahabu kwenye ukuta wenye pambo la dhahabu, ni sehemu ya kukamilisha hatua ya kwanza iliyo husisha upande wa kulia na kushoto ya mlango huo, na utaongeza uzuri wa Atabatu Abbasiyya tukufu na kulinda uzuri wa jengo lake, sambamba na kuenzi muonekano wake wa kale wenye mvuto mzuri”.