Wito wa kushiriki katika semina itayo endeshwa kwa njia ya mtandao kuhusu faharasi za nakala-kale za kiarabu chini ya kanuzi ya mark RDA 21

Maoni katika picha
Kituo cha faharasi na kupangilia taaluma chini ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetoa wito kwa kila anayependa kujiendeleza ashiriki semina itakayo endeshwa kwa njia ya mtandao kuhusu (faharasi na kupangilia taaluma chini ya kanuni ya mark RDA 21) kupitia program ya (ZOOM Cloud Meetings) siku ya Jumanne ya mwezi (21 Dhulhijjah 1441h) sawa na (11 Agosti 2020m), itadumu siku mbili kuanzia saa kumi na moja hadi saa moja jioni, kituo kimetoa wito kwa kila anayependa kujiendeleza katika mambo ya faharasi asajili jina lake.

Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa kituo hicho Ustadh Hasanaini Mussawi, amesema kuwa: “Kituo chetu bado kinaendelea na harakati kwa njia ya mtandao, kimeandaa ratiba maalum katika kipindi hiki cha maambukizi ya virusi vya Korona, leo tunaweka mezani ratiba yenye umuhimu mkubwa ambayo ni (upangiliaji wa faharasi za kiarabu kwa mujibu wa kanuni ya mark RDA 21)”.

Akabainisha kuwa: “Mkufunzi wa semina hiyo ni mtaalam wa faharasi Ali Twalib, inalenga kujenga uwezo wa watu wanaofanya kazi kwenye sekta hiyo katika kutumia utaratibu wa kisasa zaidi na wenye mafanikio makubwa katika maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya na sehemu zingine, tumekusudia kushea uzowefu wetu”.

Akasema kuwa: “Jisajili kupitia link hii: https://us02web.zoom.us/webinar/register/WN_jyx9PcTSRgmf2gvqz29yfw

Vyeti vya ushiriki vitatumwa kwa watakao shiriki tu, (vitatumwa kwenye anuani za baruapepe zilizo sajiliwa peke yake), hakikisha unaandika majina yako kwa usahihi na unapata neno la siri la kuingilia kwenye kikao (Meeting).

Kumbuka kuwa kituo cha faharasi na kupangilia taaluma chini ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, bado kinaendelea kuratibu na kufanya harakati kwa njia ya mtandao, kutokana na kuheshimu maelekezo yanayo tolewa na idara ya afya kuhusu kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: