Ataba mbili tukufu zimeonyesha mfano wa kuadhimisha kwenye kipindi cha maambukizi ya virusi vya Korona kwa mujibu wa maelekezo ya Marjaa Dini mkuu

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya umeonyesha mfano wa kufanya maadhimisho ya Husseiniyya kwenye kipindi cha maambukizi ya virusi vya Korona, kwa mujibu wa maelekezo ya Marjaa Dini mkuu, kupitia maukibu yao ya pamoja iliyofanywa jana siku ya Jumamosi katika kusherehekea sikukuu ya Ghadiir, siku aliyo tangazwa Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s) kuwa khalifa wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Wamefanya maadhimisho ya tukio hilo kubwa kwa kuchukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, wametosheka na idadi maalum ya watumishi wa Ataba mbili takatifu.

Watumishi wa Ataba mbili tukufu walianza matembezi yao katika malalo ya Bwana wa mashahidi (a.s) wakiwa wamebeba mauwa na kuimba kaswida kuhusu tukio hilo adhim, hadi wakafika kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na wakahuisha utii wao kwa Imamu wa wachamungu na mbora wa mawasii Ali bun Abu Twalib (a.s).

Watumishi wa Ataba mbili takatifu wakakusanyika karibu na kaburi la Bwana wa mashahidi (a.s) na wakamuomba Mwenyezi Mungu alipe amani na utulivu taifa la Iraq na aliondolee kila aina ya balaa.

Kumbuka kuwa jana siku ya Jumamosi mwezi kumi na nane Ddhulhijjah, ilikuwa sikukuu ya Idhul-Ghadiir siku ambayo Mtume Muhammad (s.a.w.w) alipewa amri na Mwenyezi Mungu mtukufu ya kumtangaza Ali bun Abu Twalib (a.s) kuwa khalifa, wasii, Imamu na kiongozi baada yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: