Kwa picha: Shuhudia sehemu iliyotiwa dhahabu na mlango wa Kibla katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu jana mwezi (18 Dhulhijjah 1441h) sawa na tarehe (8 Agosti 2020h) ilifanya ufunguzi wa mradi wa upanuzi wa mlango wa Kibla katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ndani, baada ya kuuweka nakshi na mapambo ya kiislamu, pamoja na mradi wa matengenezo na uwekaji wa dhahabu kwenye ukuta unaobeba pambo kubwa la dhahabu linalojulikana kwa jina la (sega), ufunguzi huu ni sehemu ya kuadhimisha sikukuu kubwa ya Idul-Ghadiir.

Nakshi na mapambo ya kiislamu yamechaguliwa kwa umakini mkubwa, ili kuonyesha utukufu wa sehemu hii kwa mtu anayekuja kufanya ziara, kutokana na vionjo vya kitaalamu kati ya nakshi na mapambo pamoja na muingiliano wa rangi, kwa namna ambayo inaendana na jengo la Atabatu Abbasiyya takatifu, hivyo mlango wa Kibla umekuwa bora kushinda milango yote ya Ataba kutokana na vile ulivyo sanifiwa.

Kuhusu sehemu iliyotiwa dhahabu ambayo imefunguliwa baada ya kufanywa kazi kubwa iliyopita katika hatua tofauti, miongoni mwa hatua hizo ni kuweka dhahabu upande wa kulia na kushoto ambayo iliongeza uzuri wa eneo hilo, sambamba na kubakiza muonekano wake wa zamani.

Kumbuka kuwa shirika la ujenzi la ardhi takatifu ndio mtekelezaji wa miradi hii, mkuu wa shirika hilo Mhandisi Hamidi Majidi amesema kuwa: “Mlango wa Kibla katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) umekuwa na uzuri wa pekee, tumezingatia mambo mengi katika kuutengeneza, ikiwa ni pamoja na jengo tukufu la Ataba takatifu, sambamba na uwiyano wa nakshi na mapambo ya milango, kuhusu kutia dhahabu ukuta wenye pambo kubwa la dhahabu kazi hiyo imekamilisha kazi iliyofanywa katika hatua ya kwanza ya kutengeneza upande wa kulia na kushoto wa eneo hilo, sehemu hiyo imeonyeza uzuri wa jengo pamoja na kuzingatia muonekano wake wa zamani”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: