Kikosi cha Abbasi kinaendelea na kazi ya kuosha na kuzika makumi ya watu wanaokufa kwa Korona

Maoni katika picha
Wahudumi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdu Shaábi) wanaendelea kuosha na kuvisha sanda watu wanaokufa kwa Korona katika kituo cha “Yaasiin” tangu kituo hicho kilipo anza kazi tarehe (20) Julai, idadi ya maiti zilizo oshwa kwenye kituo hicho hadi sasa imefika (124).

Mjumbe wa kamati inayo simamia uoshaji Ali Abdurahim Ahmadi amesema kuwa: Upokeaji wa maiti unafanywa kwa kuwasiliana na idara ya afya ya mkoa wa Karbala, kazi ya kuosha, kuvisha sanda na kuzika zinafanywa bure, akasema: “Wahudumu hawataki kupokea pesa au zawadi yeyote kutoka kwa wafiwa kwa sababu kazi hii wamejitolea kuifanya kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu pamoja na kuwatumikia raia wetu watuufu katika mazingira haya magumu, sio kwa ajili ya kutafuta hela au zawadi”.

Ndugu waliofiwa na jamaa zao kwa maradhi ya Korona wamesifu huduma zinazo tolewa na kituo hicho, pamoja na muamala mzuri kuanzia kwenye kupokea maiti, kumuosha, kumvisha sana kumswalia na hadi kumzika, pamoja na majemedari hao kuwa karibu na wafiwa na kuwaliwaza kwa kupoteza mpenzi wao, bila kujali ugumu wa kazi yao na jinsi wanavyo hatarisha maisha yao kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wa Iraq, wamesisitiza kuwa huduma zote zinatolewa bure kabisa, wanamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awalinde majemedari hawa shupavu na aondoe haraka hili janga.

Kumbuka kuwa kikosi kiliunda kamati ya kupambana na maambukizi ya korona mara tu baada ya kutokea tatizo hilo, kamati hiyo imefanya kazi ya kupuliza dawa sehemu mbalimbali hususan katika maeneo ya makazi ya watu, ndani na nje ya mji wa Karbala, inafanya kila iwezalo katika kupambana na janga hili, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kituo hiki cha kuosha, kuvisha sanda na kuzika watu waliokufa kwa ugonjwa wa Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: