Mganga mkuu wa Baabil amesema kuwa: Jengo la Alhayaat la saba linajengwa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika mapambano yake dhidi ya virusi vya Korona

Maoni katika picha
Mganga mkuu wa Baabil Dokta Muhammad Hashim Jafari ametembelea mradi wa jengo la Alhayaat la saba, linalo jengwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha usimamizi wa kihandisi kama sehemu ya kusaidia sekta ya afya kupambana na virusi vya Korona.

Jafari na wajumbe aliofuatana nao katika ziara hiyo akiwemo kiongozi wa mji huo (ambae mradi unajengwa katika eneo lake) wamesikiliza maelezo kwa ufupi kuhusu maendeleo ya ujenzi kutoka kwa wasimamizi wa ujenzi huo, pamoja na hatua kubwa waliyo piga ndani ya muda mfupi japokuwa kuna mazingira magumu, amesisitiza kuwa wanapambana na changamoto kuhakikisha wanamaliza ujenzi haraka iwezekanavyo, kutokana na umuhimu wake kwa watu walioambukizwa virusi vya Korona katika mkoa wa Baabil, nae mganga mkuu akatoa shukrani za dhati kwa Atabatu Abbasiyya tukufu na watumishi wake hususan wanaofanya kazi kwenye mradi huu, kazi hii inaonyesha wazi uwajibikaji katika jamii kwa ajili ya kusaidia wananchi watukufu wa Iraq, na unachangia kuleta matumaini ya kujinasua na janga la Korona.

Kazi inaendelea sehemu zote tatu za mradi huu, unaojengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita (3500) katika eneo la kitongoji cha Marjani cha kitabibu, jengo linavyumba (98) vya wagonjwa na zaidi ya vyumba (25) vya madaktari, wauguzi na ofisi, kazi imepiga hatua kubwa sana, kuangalia maendeleo ya ujenzi na maelezo zaidi fungua link ifuatayo: https://alkafeel.net//projects/view.php?id=94

Kumbuka kuwa jengo hili ni moja ya majengo matatu yanayo jengwa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kwenye mkoa wa Bagdad, Muthanna na Baabil, aidha ni sehemu ya vituo vinne vilivyo jengwa siku za nyuma, viwili katika mji wa Imamu Hussein (a.s) wa kitabibu na kimoja katika hospitali kuu ya Hindiyya huku kituo cha nne kilijengwa kwa ufadhili wa hospitali ya kiongozi wa waumini (a.s) katika mkoa wa Najafu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: