Kamati ya kupambana na maambukizi chini ya idara ya ustawi wa jamii katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza kupuliza dawa kwenye vituo vya kufanyia mitihani

Maoni katika picha
Idara ya ustawi wa jamii chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kuwa, kamati yake ya kujikinga na maambukizi imeanza kupuliza dawa kwenye vituo vya kufanyia mitihani, kutokana na kukaribia kipindi cha mitihani ya wanafunzi wa sekondari (upili).

Sehemu ya kwanza iliyo anza kupulizwa dawa ni sehemu za kitalii katika mkoa wa Baabil, kiongozi wa kamati hiyo amesema kuwa kazi ya kupuliza dawa, ni moja ya kazi nyingi zinazofanywa na idara yetu kwenye mikoa tofauti, sambamba na harakati zingine zilizo anza kufanywa mara tu baada ya kutangazwa maambukizi ya virusi vya Korona.

Akaongeza kuwa: Opresheni ya kupuliza dawa imepewa jina la (opresheni ya Alkafeel), pamoja na maeneo mengine, opresheni hii inalenga vituo vya kufanyia mitihani wanafunzi wa sekondari (upili), ili kuwawezesha kufanya mitihani katika mazingira salama, shughuli hii inafanywa kwa kuwasiliana na idara za shule, tayali tumesha puliza vituo vingi na kazi bado inaendelea hadi tumalize vituo vyote.

Akamaliza kwa kusema: “Tunaendelea kufanya kazi hii ya kujitolea kwa ajili ya jamii, tunatoa wito kwa kila mtu aheshimu na kufanyia kazi maelekezo ya wizara ya afya ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: