Wizara ya viwanda: ufundi na ubunifu wa kiiraq ni mradi bora katika sekta ya utafiti wa kielim unaofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu.

Maoni katika picha
Wizara ya viwanda kupitia mtaalamu wake wa maswala ya kielimu Ustadh Ammaar Abdullahi Hamdu imesema kuwa, ufundi na ubunifu wa kiiraq ni mradi unaotekelezwa na wataalam wa kituo cha faharasi na kupangilia taaluma chini ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, mchango wake unasaidia kuendeleza tafiti za kielimu.

Hayo yapo kwenye barua iliyotumwa Atabatu Abbasiyya, miongoni mwa ujumbe ulioandikwa pia ni: “Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa kituo cha faharasi na kupangilia taaluma, kwa kazi kubwa ya kitaalamu inayosaidia kuimarisha sekta ya viwanda hapa Iraq”.

Akasisitiza kuwa: “Kuna nia ya dhati ya kuimarisha ushirikiano katika mambo ya kielimu na kitamaduni, utakao leta maendeleo katika taifa letu kipenzi, tunatarajia kuendelea kufanya kazi pamoja na jopo la wawakilishi wa wizara katika kufanikisha mradi na kukamilisha hatua ya mwisho na kuufanya kuwa mradi bora kwenye sekta hiyo hapa Iraq”.

Kumbuka kuwa kituo cha faharasi na kupangilia taaluma kwa kushirikiana na wizara ya viwanda na madini walifungua mtandao wa kielimu unaosimamia ufundi na ubunifu wa raia wa Iraq, na kuuwakilisha kwenye sekta husika kwa ajili ya kunufaika nao, pamoja na kukusanya matokeo ya tafiti za kielimu na kuyapangilia sambamba na kuyahifadhi, ushirikiano huo ulianza baada ya Atabatu Abbasiyya kupokea maombi kutoka wizara ya viwanda ya kushirikiana nayo na kubadilishana uzowefu, kwa maelezo zaidi fungua link ifuatayo: http://www.iiir-mim.gov.iq/xmlui/
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: