Mkuu wa Darul-Kafeel ya uchapaji na usambazaji amesema kuwa: tunaongeza uzowefu wetu pamoja na idara ya uchapishaji wa habari ya Iraq

Maoni katika picha
Mkuu wa Darul-Kafeel ya uchapiji na usambazaji Ustadh Farasi Hakim Ibrahimi amesema kuwa tunajitahidi kuongeza mafanikio yaliyo patikana mwaka jana kwa kushirikiana na idara ya uchapaji wa habari ya Iraq, kwa kuandaa mpangokazi wa pamoja katika mradi wa kitaifa uitwao (Uchapaji nchini Iraq), utakao chapisha zaidi ya vitabu milioni themanini vya aina (22) vilivyopo katika silabasi ya wizara ya malezi, vyenye ubora mkubwa sawa na vinavyo chapishwa nje ya Iraq, tumechangia kuchapisha vitabu vya kufundishia ndani ya muda mfupi kabla ya muda uliokuwa umepangwa kwa siku (15).

Hayo yameelezwa katika ziara iliyofanywa na ugeni kutoka idara ya habari ya Iraq ndani ya ofisi za Daru katika mkoa mtakatifu wa Karbala, kuangalia vifaa kazi vilivyopo katika kituo cha uchapishaji, akasema: “Hakika ziara hii inalenga kuimarisha ushirikiano kati ya vituo viwili vya uchapishaji, ili kuendelea kufanya kazi kwa pamoja katika mradi wetu wa kitaifa na kulinda mafanikio yake, miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana ni:

  • - Kuhuisha msemo wa (Kimechapishwa Iraq) msemo huo tulikaribia kuusahau kabisa.
  • - Kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira, kwa kutoa kazi kwa kundi kubwa la watu.
  • - Kusaidia taifa na wizara ya malezi bila kuangalia faida binafsi sambamba na ubora wa machapisho unaompa amani mtumiaji.
  • - Vitabu vinawasili kwa wakati muwafaka na vinaubora mkubwa kwa matumizi ya mwanafunzi wa Iraq.
  • - Kugundua uwezo na vipaji vya vijana.
  • - Uzowefu umeonyesha kuwa taasisi za hapa nchini zikiongozwa vizuri na kuwezeshwa, zinaweza kuleta maendeleo makubwa katika taifa la Iraq.

Mjumbe wa baraza bwana Hakim Jaasim akasema kuwa: “Ziara yetu katika kituo cha uchapishaji cha Alkafeel inalenga kufungua milango ya ushirikiano katika uchapaji wa vitabu vya masomo na kuendeleza uzowefu wetu ulio onyesha mafanikio ya wazi ambao ni sehemu ya mradi wa (kimechapishwa Iraq), katika hatua ijayo tutaendelea kufanya kazi kwa ushirikiano, kutokana na kuhisi kuwajibika na uzalendo wa kulinda vituo vya uchapishaji vya Iraq, na kuacha kutegemea uchapishaji wa nje ya taifa”.

Mwishini mwa ziara yao walifanya kikao na makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Abbasi Mussa, ambae amebariki ushirikiano huo na kuomba waendelee kufanya kazi pamoja na kulinda mafanikio yaliyo patikana.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: