Chuo kikuu cha Ummul-Banina cha kielektronik cha wasichana kimetangaza ratiba ya mwezi wa Muharam

Maoni katika picha
Kutokana na kukaribia mwezi mtukufu wa Muharam wa mwaka 1442h, chuo kikuu cha Ummul-Banina (a.s) cha kielektronik cha wasichana chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetangaza ratiba yake katika mwezi huo itakayo tekelezwa kupitia mitandao ya mawasiliano.

Maelezo ya ratiba hiyo yametolewa na mkuu wa chuo Shekh Hussein Turabi: “Ratiba hii inalenga harakati maalum za chuo katika mwezi mtukufu wa Muharam”.

Akafafanua kuwa: “Ratiba hiyo itakuwa na mashindano yafuatayo:

  • 1- Shindano la (Aljuud) kaswida zinazo muelezea Abulfadhil Abbasi (a.s).
  • 2- Shindano la (Mubaligh wa Husseiniyya na jamii) wanafunzi wa chuo kikuu cha Ummul-Banina (a.s) wataandika Makala kuhusu (Nafasi ya Mubaligh wa Husseiniyya katika kutengeneza jamii kifikra).
  • 3- Shindano la (Mafundisho ya Husseiniyya ya Islahi)
  • 4- Shindano la (Hussein na Quráni).
  • 5- Shindano la (Mwangaza wa Ashura).

Unaweza kufuatilia kupitia ukurasa wa:

  • 1- Facebook
  • 2- instagram
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: