Kwa nadwa ya njia ya mtandao: Maktaba ya wanawake inaangazia umuhimu wa masomo kwa watu wenye mahitaji maalum

Maoni katika picha
Idara ya maktaba ya wanawake chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeratibu nadwa kwa njia ya mtandao inayo angalia umuhimu wa masomo kwa watu wenye mahitaji maalum, kupitia program ya (tunaendeleza maarifa kwa pamoja) ambayo shughuli zake zinafanywa kwa njia ya mtandao kutokana na kuwepo kwa maambukizi ya virusi vya Korona.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na kiongozi wa maktaba hiyo bibi Asma Al-Abadi: “Imefanywa kwenye jukwaa la maktaba katika mtandao wa kimataifa Alkafeel –mtandao rasmi wa Atabatu Abbasiyya tukufu- chini ya usimamizi wa mkuu wa Maahadi ya Alkafeel ya watoto wanaoweza kusoma chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu Ustadhat Sara Hafari, katika nadwa hiyo yamejadiliwa maswala ya akili, nafsi na mwili na kuangalia changamoto za kundi hilo na namna ya kuzitatua”.

Akaongeza kusema: “Hali kadhalika kulikuwa na maoni muhimu, miongoni mwa maoni hayo yalitolewa na Ustadh Osama Khatwabi, alibainisha umuhimu wa kusaidia taasisi za kijamii kwa hali na mali, misaada ya mali inajumuisha majengo, sekta ya afya, huduma ya umeme, usafi na kuweka mazingira rafiki kwa kutumia watu wa mazingira, ili kufanya mazingira kuwa salama na safi kwa kila mtu na kuhakikisha mahitaji yote ya msingi yanapatikana, ili kumfanya mtoto awe na makuzi sahihi kinafsi, kiafya na kimwili”.

Akamaliza kwa kusema: “Nadwa imepata mwitikio mkubwa na ushiriki hai, uliopelekea kuongeza kuda uliokuwa umepangwa, kutokana na umuhimu wa mada zilizokuwa zikiongelewa kuhusu kundi hilo ambalo lazima lipewe uangalizi maalum ili liweze kufanikiwa na kuonyesha uwezo wake, na liwezo kuchangia uchumi wa jamii na taifa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: