Mwanafunzi aitwae Raghada Abdulkarim, mmoja wa wanafunzi wa Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wasichana, chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, amekuwa mshindi wa nane kwa kupata alama (95.5) katika shindano la kuhifadhi surat Baqarah lililo endeshwa kimtandao kwa mara ya kwanza.
Hayo yamesemwa na mkuu wa Maahadi bibi Manaar Jawadi Jiburi: “Hili ni moja ya mashindano ambayo wameshiriki wanafunzi wa Maahadi na kupata nafasi za juu, kutokana na mazingira ya sasa ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona tunatumia njia ya mtandao, ikiwa ni pamoja na shindano hili ambalo lilikuwa na washiriki zaidi ya (120) kutoka nchi tofauti pamoja na Iraq”.
Kumbuka kuwa hii sio mara ya kwanza kwa wanafunzi wa Maahadi tawi la wasichana kushiriki na kupata nafasi za juu, wamesha shiriki mashindano mengi na kupata nafazi hiyo, hii inaonyesha ubora wa silabasi ya Maahadi na umakini wa idara yake.