Muhammad na Ibrahim ni watoto wa balozi wa Imamu Hussein Muslim bun Aqiil bun Abu Twalib (a.s), watoto hao walikuwepo katika vita ya Twafu, tukio lao halikufanyika baada ya saa chache au siku chache bali baada ya mwaka mzima na kuleta mshtuko mkubwa, mwezi ishirini na tatu ya Dhulhijjah ni kumbukumbu ya kifo cha watoto hao ambayo inaweza kuchukua nafasi ya pili kwa ukubwa wa dhulma waliyo fanyiwa, baada ya kuuwawa Imamu Hussein (a.s) pamoja na watoto wake, ndugu zake na wafuasi wake katika ardhi ya Karbala.
Kwa mujibu wa historia Muhammad na Ibrahim walikuwa na Imamu Hussein (a.s) Karbala, wakatengana na familia ya Imamu baada ya mauwaji ya Karbala, wakatekwa na utawala wa Ubaidullahi bun Ziyadi kwa muda wa mwaka mzima takriban.
Baada ya kufanikiwa kwao kutoroka jela, mmoja wa vibaraka wa utawala aliye hadaika na zawadi nono iliyokuwa imeahidiwa na utawala kwa atakae wakamata, aliwakamata na akaenda nao hadi pembeni ya mto Furaat, walipo gundua kuwa anaenda kuwauwa walimuambia: Ewe Mzee..! tuuze sokoni na utapata pesa –walimuambia hivyo ili afanikishe lengo lake la kupata mali-, lakini alikataa na kuendelea na nia ya kuwauwa pamoja na kwamba walimuambia wazi kuwa wao ni katuka watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w)!! aliwaambia: mimi nakuuweni na nitaenda kuchukua zawadi nono kwa kufanya hivyo, wakamuambia: basi tupeleke tukiwa hai kwa ibun Ziyadi atuhukumu yeye mwenyewe, yule mzee akakataa hilo pia, akawachinja bila huruma pembeni ya mto wa Furaat, miili yao mitakatifu akaitupa mtoni na kubeba vichwa vyao.
Riwaya zinasema mtu huyo muovu alimchinja mtoto mkubwa, yule mdogo akajipaka damu za kaka yake na akasema: nitakutana na Mtume wa Mwenyezi Mungu nikiwa hivi nimelowana damu ya kaka yangu, kisha akakata kichwa chake na akatupa mwili wake mtoni, akabeba vichwa vya watoto hao na kuvipeleka kwa ibun Ziyadi halafu akamuhadithia kilicho tokea baina yake na wale watoto, ibun Ziyadi alichukizwa na tukio hilo na akamnyima zawadi halafu akaamuru auwawe kwa ukatili aliofanya.
Makaburi ya watoto hao yapo umbali wa kilometa tatu mashariki ya wilaya ya Mussayyab, upande wa mashariki ya mto Furaat, eneo hilo kiofisi lipo chini ya mji wa Hilla katikati ya Iraq.