Idara ya ustawi wa jamii imejitolea kujenga nyumba na kuweka vifaa vya ndani kwa ajili ya familia moja iliyopo kwenye mazingira magumu mjini Bagdad

Maoni katika picha
Mawakibu za kutoa misaada chini ya idara ya ustawi wa jamii katika Atabatu Abbasiyya tukufu, hazijaishia kwenye kusaidia wapiganaji peke yake, japokuwa hilo ndio jukumu lao la msingi na ndio sababu ya kuanzishwa kwake, kazi zao zimesambaa hadi katika maeneo mengine kutokana na mazingira ambayo watu wanaishi, zimekuwa zikitoa misaada ya aina mbalimbali, ukiwemo msaada huu uliotolewa na maukibu katika mji wa Bagdad, kujenga na kuweka vifaa vya ndani kwa ajili ya familia moja ya watu wanaoishi kwenye mazingira magumu.

Kiongozi wa maukibu bwana Swadiq Saaidiy amesema kuwa: “Ni utukufu kwetu kusaidia shida za raia wetu na kuingiza furaha katika nyoyo zao baada ya kukata tamaa, baada ya kuangalia mazingira ya familia hii tumeamua kuwajengea nyumba inayo endana nao kwa kushirikiana na kikosi cha furaha kwa mayatima, tumewajengea nyumba ambayo itawafanya waishi vizuri, hatukuishia kujenga nyumba peke yake bali tumenunua na vyombo vya ndani na kuweka kila kinacho hitajika katika nyumba”.

Kumbuka kuwa nyumba hii sio ya kwanza kujengwa, zimesha jengwa nyumba nyingi kama hiyo kwa ajili ya familia zinazo ishi kwenye mazingira magumu, familia za mashahidi na familia za watu wenye mahitaji maalum katika mji mkuu wa Bagdad na mikoani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: