Siku ya Mubahala ni siku shuhudiwa na msingi mkuu wa mfululizo wa siku za kiislamu

Maoni katika picha
Mwezi wa Dhulhijja unamatukio makubwa, nuru ya mwezi huo imeendelea kuangaza katika ujumbe wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), likiwemo tukio la mwezi ishirini na nne mwaka wa kumi hijiriyya, tukio la kuapizana (Mubahala) kati ya Mtume (s.a.w.w) na manaswara wa Najrani.

Maana ya neno (Mubahala) kama inavyosema tafsiri mizani: “Maapizano”.

Katika riwaya iliyopo kwenye kitabu cha tafsiri Qummiy kutoka kwa Swadiq (a.s) anasema: Wakristo wa Najrani walipokwenda kwa Mtume (s.a.w.w) uliingia wakati wao wa sala, wakapiga kengele na kuswali, maswahaba wa Mtume (s.a.w.w) wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu unaruhusu jambo hili katika msikiti wako?! Mtume akasema: Waacheni. Walipo maliza kusali wakasoea kwa Mtume (s.a.w.w), wakasema: unatulingania katika jambo gani? Akasema (s.a.w.w): katika shahada ya kwamba hakuna Mungu ispokuwa Allah na mimi ni Mtume wake, na Issa ni mja wa Mwenyezi Mungu, alikuwa anakula na kunywa na kuzungumza, wakasema: baba yake ni nani? Ukateremka wahyi kwa Mtume (s.a.w.w), waulize: wanasemaje kuhusu Adam, alikuwa mja aliyeumbwa na Mwenyezi Mungu anakula, anakunywa na anazungumza na kuowa? Mtume (s.a.w.w) akawauliza. Wakasema: ndio. Mtume (s.a.w.w) akawauliza: baba yake ni nani? Wakakosa jibu (wakabutwaa), Mwenyezi Mungu mtukufu akateremsha aya inayo sema: (Hakika mfano wa Issa mbele ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam alimuumba kwa udongo kisha akasema kuwa na akawa..)

Na pindi ilipo shuka kwa Mtume (s.a.w.w) aya isemayo: (Watakao kuhoji katika hili baada ya kukufikilia elimu hii waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wake zetu na wake zenu, na sisi wenyewe na nyinyi wenyewe, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo) hiyo ndio ilikuwa amri ya Mwenyezi Mungu mtukufu, Mtume (s.a.w.w) akawaambia: tuapizane.. kama nikiwa mkweli mtashukiwa na laana ya Mwenyezi Mungu, na nikiwa muongo laana itanishukia, wakasema: umesema jambo jema. Wakakubaliana kuapizana siku inayo fuata, ambayo ni mwezi ishirini na nne Dhulhijja mwaka wa 10 hijiriyya, waliporudi majumbani kwao, viongozi wao ambao ni Sayyid, Aqaab na Ahtamu wakasema: akija kuapizana na maswahaba zake tuapizane nae atakua sio Mtume, na akija na watu wa nyumbani kwake tusiapizane nae, hawezi kuja na watu wa nyumbani kwake ispokuwa atakuwa ni mkweli. Kulipo kucha, Mtume (s.a.w.w) akaenda na kiongozi wa waumini (a.s) na Fatuma na Hassan na Hussein (a.s).

Ugeni wa manaswara ukauliza: hawa ni wakina nani? Wakaambiwa: huyu ni mtoto wa Ammi yake na wasii wake Ali bun Abu Twalib, na huyu ni mtoto wake Fatuma na hawa ni watoto wa mtoto wake Hassan na Hussein (s.a), wakasema: tumekubali, tuache kuapizana. Mtume akafanya nao makubaliano ya kulipa kodi (jazya), kila mwaka watoe jola elfu mbili za nguo, jola elfu moja katika mwezi wa Safari na jola elfu moja mwezi wa Rajabu, pamoja na ngao thelathini, farasi thelathini na mishale thelathini, wakaondoka..

Tukio hili linaonyesha utukufu wa ujumbe wa Mtume Muhammad ulio onyeshwa na mtu mmoja wala sio watu wengi akiwa na mwanamke mmoja wala sio wanawake wengi, na watoto wawili wala sio watoto wengi, hao ndio watu wasafi na watakasifu wa nyoyo walio teuliwa na Mwenyezi Mungu, na akawaandaa kuongoza umma baada ya Mtume wake (s.a.w.w).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: