Shekh Hussein Turabi mkuu wa Maahadi amesema kuwa: Ratiba iliyo andaliwa inaendana na utukufu wa mwezi huo kwa siku zote tena kwa kufuata nyakati maalum, miongoni mwa vipengele vya ratiba hiyo ni:
- Hurufu Twafu: Ratiba ya mihadhara inayo elezea harakati ya Husseiniyya.
- Duraru-Mimbari: Vipande vya video za mihadhara ya Shekh Ahmadi Waailiy.
- Shairi kutoka Twafu: Ratiba ya mashairi ya tukio la Twafu.
- Matukio ya Muharam: Kuangazia mambo yaliyo tokea katika mwezi wa Muharam na Safar.
- Pamoja na wafuasi wa Hussein (a.s): Kuangazia historia ya wafuasi wa Imamu Hussein (a.s).
- Athari za kijamii kuhusu harakati za Imamu Hussein (a.s) na jinsi zinavyo athiri familia na jamii.
- Walisema kuhusu Hussein (a.s): Ratiba inayo angazia swala la Husseiniyya katika mtazamo wa Mustashriqina.
- Visa vya wanachuoni: Ratiba ya kuangalia yaliyotokea kwa wanachuoni kuhusu swala la Husseiniyya.
Fuatilia ratiba hiyo kupitia mitandao ifuatayo:
Yotube
Telegram