Shughuli za kupuliza dawa zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika vita ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona bado zinaendelea

Maoni katika picha
Tangu lilipotokea janga la Korona Atabatu Abbasiyya tukufu imeunda kamati maalum ya kupambana na janga hilo chini ya kauli mbiu isemayo (kinga ni bora kuliko tiba), miongoni mwa kazi zinazo fanywa kupambana na virusi vya Korona ni kupuliza dawa katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya mkoa wa Karbala.

Kuhusu mji wa Karbala, imeundwa kamati maalum inayo simamia shughuli za kujikinga na maambukizi inayo husisha vitengo na idara za Atabatu tukufu pamoja na kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, kamati hiyo imeweka ratiba ya utendaji wa shughuli zao, wanatumia vifaa vyenye ubora mkubwa vilivyo tengenezwa na shirika la Khairul-Juud.

Shughuli hizo ambazo bado zinaendelea hadi sasa, zilianzia katika eneo linalo zunguka haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na katika mji mkongwe na barabara za ndani ya mji huo pamoja na maeneo ya mpakani.

Kiongozi wa idara ya tiba katika Ataba tukufu Dokta Osama Abdulhassan amesema kuwa: “Tangu ilipoundwa kamati ya kupambana na maambukizi, uliandaliwa mpangokazi uliokuwa na vipengele vingi, lengo kubwa likiwa ni kuzuwia kusambaa maambukizi ya virusi vya Korona na kusimamia utekelezaji wa maelekezo ya wizara ya afya ya Iraq pamoja na shirika la afya la kimataifa, miongoni mwa shughuli zilizopo kwenye mkakati huo ni kupuliza dawa kwenye majengo yote ya Atabatu Abbasiyya pamoja na maeneo yanayo zunguka majengo hayo”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya mambo mengi katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, sambamba na kutekeleza maagizo tofauti yanayo tolewa na idara ya afya, katika ngazi ya Ataba, mji mkongwe na mkoa kwa ujumla.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: