Mazingira ya huzuni za Ashura yameanza kuonekana kwenye korido na kuta za Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Tunakaribia kidogo kidogo katika mwezi wa huzuni za Ahlulbait (a.s) na wafuasi wao pamoja na wapenzi wao, katika kumbukumbu ya kuuwawa Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake pamoja na wafuasi wake (r.a), mazingira ya huzuni yameanza kuonekana kwenye korido na kuta za Ataba ya mbeba bendera ya Twafu Abulfadhil Abbasi (a.s), watumishi wa kitengo cha uangalizi wa haram ya Atabatu Abbasiyya wameanza kuweka alama za kuomboleza, baada ya kitengo cha ushonaji kumaliza kushona vitambaa vinavyo ashiria huzuni.

Hayo yamesemwa na makamo rais wa kitengo hicho Ustadh Zainul-Aabidina Quraishi: “Watumishi wa kitengo chetu wanamajukumu mengi, kuna yanayo onekana na yasiyo onekana, miongoni mwa kazi tunazo fanya ni kuweka muonekano wa mazingira ya huzuni katika siku za kuomboleza kifo cha Imamu miongoni mwa maimamu wa Ahlulbait (a.s), kikiwemo kifo cha bwana wa Mashahizi Imamu Hussein (a.s), ambacho ni msiba mkuwa zaidi kutokana na kauli ya Imamu Hassan (a.s) isemayo: (Hakuna siku “chungu” kama siku yako “utakayo uwawa” ewe Abu Abdillah), na Imamu Swadiq (a.s) anasema: (Unapoingia mwezi wa Muharam malaika hukunjua kanzu ya Hussein (a.s) ikiwa imelowa damu, sisi na wale wanaotupenda huiona kwa moyo sio kwa macho, huingia katika hisia zetu na kuhuzunisha nafsi zetu..”.

Akafafanua kuwa: “Kazi zetu huanza siku kadhaa kabla ya kuingia mwezi wa Muharam na huendelea hadi mwisho wa mwezi, huwa tunafunga vitambaa vyeusi na kuweka mabango yaliyo tengenezwa na idara ya ushonaji, chini ya kitengo cha zawadi na nadhiri katika Atabatu Abbasiyya tukufu, baada ya kuchukua vipimo vya sehemu zote, milangoni, kwenye nguzo, ndani na nje ya haram takatifu, kwa kutumia vitambaa vyenye ubora mkuwa, kila kitambaa hushonywa kulingana na sehemu kinapo kwenda kuwekwa, bila kuharibu sehemu kinapo wekwa, kwani huwekwa kwa kutumia gundi maalum ambayo huwa rahisi utowaji wake”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: