Shughuli za kuomboleza Ashura kwa vikundi vya Karbala zitagawanyika sehemu mbili katika mazingira haya ya janga la Korona

Maoni katika picha
Mjumbe wa kamati inayofuatilia mawakibu Husseiniyya Ustadh Jawadi Hasanawi amesema kuwa, shughuli za kuomboleza Ashura ambazo hufanywa na mawakibu pamoja na vikundi vya Husseiniyya vya Karbala zitakuwa za aina mbili, kutokana na mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona.

Akasema: “Kutakuwa na shughuli za maombolezo kila siku chini ya usimamizi mkali wa kutekeleza maagizo ya idara ya afya kuhusu namna ya kujikinga na maambukizi”.

Akafafanua kuwa: “Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimefanya kikao na wawakilishi wa vikundi vya uombolezaji, na wamefanya makubaliano maalum, kubwa ikiwa ni kugawa sehemu mbili shughuli za uombolezaji na kutekeleza maelekezo ya idara ya afya kulingana na mazingira ya sasa”.

Akasema: “Tumeweka ratiba maalum ya uingianji wa mawakibu itakayo anza siku ya kwanza ya mwezi wa Muharam, zitaruhusiwa maukibu mbili tu tena zenye idadi maalum ya watu kila siku, chini ya utekelezaji wa maagizo yote ya idara ya afya, ikiwa ni pamoja na kuzingatia umbali kati ya mtu na mtu pamoja na kuvaa barakoa”.

Akaongeza kuwa: “Ratiba tuliyokubaliana kwenye kikao inamakundi mawili, yatakayo fanya maombolezo katika eneo la katikati ya haram mbili, kundi la kwanza litafanya siku za (2 – 4 – 6 – 8) ambao watakuwa upande wa Abbasiyya na kutumia mlango wa Khaani, Twaaq na Salalima, hilo ni kundi la Swafariin na Mukhayyam, kundi la pili litatumia mlango wa Bagdad, Jumuiyyah, Najafu, Balushi, Iskani, mji wa Abbasi na siku zake ni (3 – 5 – 7 – 9)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: