Mapambo 14 yamependezesha paa na ukuta wa mlango wa Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Watumishi wa idara ya mapambo chini ya kitengo cha usimamizi wa haram ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wamemaliza kuweka mapambo kwenye paa ya mlango wa Kibla katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ndani, pamoja na ukuta uliowekwa tofali za mapambo ya ukutani pande mbili za mlango, kazi hizo ni sehemu ya mradi wa upanuzi wa mlango wa Kibla wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ndani, sambamba na kuweka nakshi na mapambo ya kiislamu, kazi hiyo ilikamilika wiki iliyopita.

Ili kutambua zaidi kuhusu mapambo hayo tumeongea na kiongozi wa idara Ustadh Hussein Abdurabi, amesema: “Mapambo yaliyowekwa kwenye paa ya mlango wa Kibla yamefika (14), kwenye kila usawa wa kubba zilizopo katika paa hilo zinazo ashiria maasumina kumi na nne (a.s) tumeweka pambo. Mapambo mawili yapo usawa wa mlango yenye taa (25) zenye urefu wa (sm180) na upana wa (sm97), mapambo mengine kumi na mbili taa zake zinaurefu wa (sm96) na upana wa (sm180) huki kila moja likiwa na taa (25)”.

Akaongeza kuwa: “Ukuta umewekwa tofali za mapambo (12) zenye urefu wa (sm76) na upana wa (sm63) zikielekea nje kwa (sm90), kila moja inataa (12) upande wa kulia na kushoto, na katikati ya upande wa juu kunamapambo ya upinde kwa ndani yapatayo (12)”.

Akasisitiza kuwa: “Mapambo yaliyo wekwa yanaendana na mapambo yaliyopo ndani ya haram takatifu, kwa ajili ya kuweka uwiyano baina ya mapambo haya na yale yaliyopo ndani na nje ya haram”.

Kumbuka kuwa mapambo haya yameletwa kutoka jamhuri ya Tashiki, inayo sifiwa kwa kutengeneza mapambo ya kifahari, mapambo haya yametengenezwa kwa (BRILLANT CRYSTAL LIGHTING), katika shirika lenye uzowefu mkubwa wa kutengeneza mapambo ya aina hii, na yalitengenezwa rasmi kwa ajili ya Atabatu Abbasiyya sambamba na kubaini sehemu litakapo wekwa kila pambo kwa ajili ya kuzingatia uzito, nakshi, utumiaji wa umeme na mengineyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: