Upasuaji wa aina yake: kwa ajili ya kurekebisha mfupa wa jicho la kijana mwenye miaka zaidi ya thelathini katika hospitali ya Alkafeel

Maoni katika picha
Jopo la madaktari wa hospitali ya rufaa Alkafeel limefanikiwa kumtibu kijana mwenye umri wa zaidi ya miaka thelathini aliyekuwa na tatizo la kupasuka mfupa wa jicho.

Daktari bingwa wa upasuaji wa uso katika hospitali hiyo, Dokta Ridhwani Twaaiy amesema kuwa: “Jopo la madaktari chini ya usimamizi wetu limefanikiwa kuunganisha mfupa wa jicho kwa kutumia picha za mionzi”.

Akaongeza kuwa: “Mgonjwa anaumri wa miaka (32) alivunjika mfupa wa jicho katika ajali”.

Akafafanua kuwa: “Hospitali ya Alkafeel ina vifaatiba vya kisasa na maabara zenye ubora wa kimataifa, jamba hilo limetuwezesha kufanya upasuaji mbalimbali kwa mafanikio makubwa”.

Tambua kuwa Hospitali ya rufaa Alkafeel hutoa huduma wakati wote kutokana na kuwa na vifaatiba vya kisasa pamoja na madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya nchi, jambo linalo ifanya kuwa na huduma za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa kila baada ya muda sambamba na kupokea wagonjwa wa aina tofauti waliopo katika hali mbalimbali za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: